“A” | Frequency ya dunia, Sadaka na mambo ya utamaduni,
baada ya kujifunza mambo mengi kwenye sura tatu zilizopita sasa tuangalie, Frequency ya dunia, Sadaka na mambo ya utamaduni kwenye sura ya nne ya kitabu cha MITETEMO YA KIROHO .
Katika sura hii tunaingia kwenye uwanja mpana unaounganisha Nguvu ya Dunia, mila, sadaka, na utamaduni, tukivivua katika mwanga wa Sheria ya Frequency. Kila jamii duniani imekuwa na mbinu zake za kuwasiliana na mizimu, kuponya roho, na kutuliza mababu. Hapa tunafungua siri ya kiini cha tamaduni hizi—frequency.
1. Frequency ya Dunia: Je, Dunia Inaishi Kimuujiza?
Ndiyo. Duniani kuna frequency maalum zinazotiririka kila mahali kama mapigo ya moyo jina maarufu Schumann Resonance – 7.83 Hz, Frequency hii ni “moyo wa Dunia.” Inaungana moja kwa moja na mawimbi ya ubongo ya Theta (4–7 Hz) frequency ya utulivu, uponyaji na mawasiliano ya kiroho. Ndiyo maana watu wanapotembea misituni, ufukweni, au vilimani wanahisi kuwa tofauti,wametulia, mawazo wazi, bila msongo
Hii ni kwa sababu Beta (stress) inashuka, na Theta (utulivu) inapanda.
Maeneo ya Low Frequency (Vortex za Uchungu)
Kuna maeneo duniani yaliyopitia matukio kama, Vita, Mauaji, Kuteswa, Mikosi mikubwa. Matukio haya huacha alama ya Low Frequency, ambayo huvuta roho wasumbufu na mawimbi ya hofu/hasira. Hakuna kitu cha ajabu—ni sayansi ya frequency.
Maeneo ya High Frequency (Sacred Sites)
Haya ni maeneo ambapo: Maombi hufanywa, Hekalu limejengwa, Asili haijaharibiwa, Watu hutafakari kwa amani(meditation). Hapa frequency huwa juu sana, inaweza kuponya mwili, kuboresha mtazamo wa kiroho, na kufungua intuition.
2. Frequency na Sadaka / Dawa za Jadi
Utamaduni wa Kiafrika na wa mababu haukuwahi kuwa “uchawi tu”—ulikuwa mfumo wa frequency. Sadaka, kuchinja, mitishamba, na hata viungo vya wanyama vina misingi ya frequency.
A. Sadaka – Kipaumbele cha Kushusha au Kupandisha Frequency
Sababu ya Sadaka (Kuchinja) Kiroho
Mababu wenye mizigo ya Low Frequency wanakuwa na Njaa ya kiroho, Hasira, Majuto, Tamaa, Makovu ya maisha, Deni za familia na wanaweza kuendelea kuathiri kizazi. Hivyo kuchinja hutumika kama: Kutoa nishati ya maisha (Life Force), Kulisha frequency ya roho iliyokwama, Kutengeneza utulivu wa muda. Haya ni malipo ya kimawimbi, si lazima ishara ya upendo.
B. Mitishamba & Viungo vya Wanyama
Mitishamba
Mmea una frequency yake ya uponyaji na frequency hiyo inaweza kuendana na mawimbi ya Dunia—Theta (Schumann). Ndiyo maana: Hutuliza, Hupunguza magonjwa (Low Frequency), Hurekebisha chakras
Viungo vya Wanyama
Waganga hutumia kwa sababu mnyama hubeba frequency ya: Ujasiri, Ulinzi, Kasi, Nguvu na Zinaweza kutumika kuongeza High Frequency (mganga mweupe) au Low Frequency (uchawi mweusi).
C. Waganga wa Jadi na Mababu
Waganga huingia kwenye: Alpha naTheta na hapo ndipo wanawasiliana na Mababu Wema, Roho wa Asili, Nature Spirits na wote Hawa huongoza jinsi ya kutumia miti, mizizi, majani, au dawa za mwili.
Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 ,
BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPA
TA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO

0 Comments