Jinsi akili ilivyo chanzo cha frequency yako

 Akili Yako: Chanzo Kikuu cha Frequency Yako.



Inaweza kuwa ngumu sana kupambana na akili yako, kama haufahamu jinsi akili inavyo asili hisia yako baada ya ama umesababishiwa au harakati za maisha zimesababisha. Ubongo wako hutuma mawimbi (Brainwaves) yanayoamua jinsi unavyotulia, jinsi unavyofikiri, jinsi unavyoamini, jinsi unavyounda ukweli. Kuna muda akili ina tuma au kupokea aina ya mawimbi ambayo ni ya Stress(Beta) inaweza kuwa stress yoyote ile mawimbi haya ni mazuri sana kwa ajili yanatusaidia kufanya maamuzi ya haraka katika ulimwengu wa vitu vinavyo onekana na vinavyo shikika, ndio inatupa utimamu wa kimantiki. Mawimbi haya hutegemea sababu ndio kupeleka ishara ya kujenga maamuzi, bila sababu amna tendo. Mfano umeona nyoka , kwenye kumbukumbu umejiwekea nyoka ni hatari basi ghafla utapata hofu, umeona moto huwezi kusogelea kwa kuwa akili inajua balaa la moto nazani umenielewa ninacho maanisha hapa kwamba mawimbi ya Beta kwenye ubongo ni sawa na hali ya papala(dholuba) yaani kukosa utulivu inahakikisha kila kinacho kuzunguka inakifahamu na kusajili hisia yake kwa ajili ya matumizi ya baadaye kama ni kipya.

Nimeeleza kwa kuzunguka ili mwenye kuelewa aelewe ,, sasa tuje kwenye mada yetu uhusiano na mambo ya frequency katika elimu ya kiroho. 


Unapokuwa kwenye hisia za huzuni, presha, mawazo ya haraka, hofu na hali zingine za namna hii,… fahamu upo kwenye Low Frequency (Beta) hali hizi zinapeleka ishara potofu kwenye Subconscious Mind(akili ya Hazina) na kumbuka nilikwambia sehemu hiyo ya ubongo katika mwili wa binadamu ni mahala patakatifu sana kwani ndio hukaa amri zote, mwili kupitia vituo vya nishati husoma zitetemeke au zitoe nishati kiwango gani kutoka hapo.

Akili ya hazina, haielewi lugha , picha, wala maneno yenyewe inaelewa frequency inayo ingia na akili hii ya hazina ndio kama kompyuta inayo amlisha mwili kupitia vituo 7 vya nishati , wakati huo Beta hutaka kujua kila sababu ya kitu ili kupeleka frequency flani kwenye akili ya hazina. Akili ya beta ndio huzoea mazingira , ndio akili inayo kuambia hivyo sio sahihi au ni sahihi kutokana na ulivyo izoeza. Mfano ulizoea kuweka kitu mahala flani siku moja kwa Bahati mbaya uka weka mahala pengine , bila utulivu ukiwa unahitaji kitu hicho utaenda mahala pale pa kila siku. Ukizoea ku vaa saa kulia siku ukijaribu kuvaa kushoto utaona kama hofu ya kutokea pasipo julikana kwamba kuna kitu hakija kaa sawa au hata kama sio hofu basi unakuwa unaona kama sio sawa yaani haujazoea, hali itaendelea kuwa hivyo hadi siku tatu au baada ya muda flani ili izoee. sasa akili ya beta kutokuelewa kwake kunakuwa kunapeleka frequency ambayo sio kwenye akili ya hazina na mwili ndio unasoma hapo kwenye akili ya hazina ndio unakuwa unapata hisia izo za kutokuzoea hali.

Akili ya beta hata kitu cha kawaida inaweza kukizuia inaweza kukwambia hicho sio kwa sababu tu , haikitambui , mfano mtu anakwambia nataka nikupe hela unakuwa hauamini hata kama ni kweli anataka akupe.

Nihitimishe kwa kusema hakuna mtu anayeweza kuridhisha akili ya Beta, ambayo inakaa kama mlinzi wako kwani isipokuwa hivyo huenda wewe unakuwa chizi.

Jifunze kuipuzia akili ya BETA maana inaweza kukupotosha hata kitu kisicho na madhara. 

Akili hiyo ya Beta huzuia uelewa wa ndani , huzia maono , kwa sababu yenyewe inatambua sana vitu halisi vya ulimwengu Wanyama, akili hiyo huzuia ubunifu, akili hii huondoa uwezo wa kuvuta picha ya kitu yaani ku imagine(zana kubwa ya kujenga picha kwenye ubongo).

Maono,ubunifu,uelewa wa ndani , uwezo wa ku imagine, ulimwengu wa hisia vyote hivi hufanyika kwenye mawimbi ya ubongo ya ALPHA(akili iliyo tulia, isiyo na papala wala dholuba) na THETA (akili iliyo tulia sana, kama maji masafi yaliyo tulia na unaweza ona kitu kilicho chini, hapa ndio watu hufumba macho akiwa anawaza chakufanya ili kuvuta picha ya ndani na kuona suluhisho na ni uhalisia huwa wanafaulu, kitu ambacho wakiongeza mazoezi wanakuwa watu hatari sana kwa maana jicho la tatu linafunguka kama ilivyo kuwa utotoni mwao)

Hapa Akili ya Hazina (Subconscious) inafunga milango yake. Hupokea ishara potofu, hutoa matokeo potofu.

Mawimbi ya akili ya BETA ni mawimbi ya akili ambayo haija tulia kabisa, Ushahidi au ukitaka kunielewa hapa ndio watu huambiwa usifanye maamuzi ukiwa ama na hasira,chuki,wivu, kwa kuwa ni rahisi kupotoka. Kwenye Mawimbi haya watu hujinyonga, hujirusha ghorofani, hujitupa visimani , hubaka, huuwa, huumiza watu kwa hasira na baadaya ya tukio kama hajafa ndio anajikuta amefanya vituko.

Mambo ya giza hushambulia watu kwa urahisi wakiwa kwenye hali hii, roho wa ukoo mbaya atakuvaa , majini watakuvaa ukiwa na hali hiyo. Makosa watu hufanya kutokufahamu hatari ya kuwa na hasira, wivu,chuki,,,,,n.k , hawafahamu kama wanakuwa kwenye frequency ya mambo ya giza kama majini, mababu wasumbufu ambao ndio sana huvaa watu na kushinikiza mambo mbalimbali waliyo wafanya wao hadi kupelekea kufa.

Hata kama sio kupelekea mtu kufa, mambo ya giza ni Pamoja na umasikini maana umasikini ni stress, unakuta babu alikufa ni masikini kwa hiyo mtu ukiwa kwenye stress za pesa (low frequency) anakuvaa na unajikuta unajikatisha tamaa ya kimaendeleo, suluhisho la hili ni kuto kuruhusu hali za low frequency. Hatua ya kwanza ni kuzifahamu na hatari zake na ndio hizi mimi naweza sema ndio shetani.

Hata wanao chinja kupata mali ni kwa ajili ya kutuma mtetemo wa kuuwa ishara ya mambo anayo nuia mtu yafe.


Sasa kwa kuelewa BETA (Low Frequency) unajukumu la kuipuzia ili kuvuka na kurefusha mna wa babeli ufike kwenye ALPHA na THETA mawimbi ya ubongo ambayo yanawezesha HEKALU TAKATIFU(akili ya azina-Subconscious Mind) kufanya kazi, 

High frequency (Utulivu)-Unapokuwa kwenye utulivu,hisia ya ubunifu,uwazi,intuition(intuition ni uelewa wandani, ile hali ya kushangaa kitu umekielewa bila nguvu), uponyaji(watu hulazwa hospitali ili wapete utulivu mwili ujiponye),mafunzo ya ndani…..fahamu kuwa mawimbi ya ubongo ya Alpha na Theta ndio yametawala katika ubongo, hapa nis awa dholuba imeisha baharini na umeshusha nanga na unaweza kupiga mbizi.

Na hapo mambo haya yanafunguka, uwezo wa roho,uelewa wa ki-mungu,mwongozo wa ndani,uponyaji wa karma.


Ukiwa kwenye High Frequency ndipo hapo tunasema Nyota yako ina waka, kwani ni muda ambao unaungana na ulinzi wa kiroho, ubunifu, kujiamini katika kila unacho kiwaza na hivyo mambo yako Kwenda kirahisi sana , kwa maana unakuwa wewe yule wewe wa ndani, nguvu yako inakuwa inavuta mtu ambaye wewe ni suluhisho lake, mfano kama unanguvu ya uponyaji , utashangaa watu wana kusimulia matatizo yao yanayo itaji uponyaji , wewe mwenyewe utashangaa kwamba huyu mtu amejuaje ??? na mchawi kazi anakuwa nayo kwa muda wote atakuwa anajiuliza huyu ujasiri anautoa wapi, nini kina mpa kiburi.


Unapo kaa kwenye hali ya high frequency muda mrefu ndio ivyo ambavyo unazoea hali hiyo na ndio hivyo naweza kufananisha na taa ambayo ipo peke yake kwenye giza na yoyote mwenye shida na mwanga hufuata mwanga. Hivyo ni jukumu lako kutoa mwanga wako.

Unapokaa kwenye high frequency kuna nishati inakuwa inakuzunguka ambayo maajabu ya kwanza utakayo yaona ni shikamoo zitaongezeka barabarani tofauti na sio kila mtu alikuwa ana salimiana na wewe, ama mtoto mdogo asiye tembea anaweza kukuona na akajiskia usalama na amani na akawa na furaha sana na wewe utapigiwa simu na watu ambao hata wamekusahau, hautakuwa unaongea sana kwa maana kabla hauja maliza kuongea mtu anakuwa ameelewa kuwa unachokisema unakiweza hata kama hauja somea.


Epuka kujiskia vibaya, penda kujiskia vizuri,,

Leo tumesoma jinsi Akili yako ilivyo chanzo kikuu chako cha frequency

Somo linalo kuja tutajifunza jinsi mwili ulivyo kioo cha frequency , au jinsi mwili ulivyo amplifier , kwamba ukipokea frequency ya ujasiri unaongeza nguvu.

Ili uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 

BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA E

LIMU HII KUBWA YA KIROHO.




Post a Comment

0 Comments