| Bonyeza picha kusikiliza sauti za Frequency |
Mwili wako ni kama kioo cha frequency huakisi frequency
inayo ingia , tendo linalo fanywa na mwili ni matokeo ya frequency iliyo ingia
, mfano unaweza kumuona mtu mwenye chuki na kitu kwa vitendo vyake kulenga kitu
au mtu huyo na hata maneno yake. Mwili huitikia na kutii frequency , mwili
hupokea frequency kutoka kwenye chanzo
kikuu(akili ya hazina) na pia hutuma frequency Kwenda kwenye akili ya hazina
kwa kupitia milango ya fahamu na hisia,mtazamo,tabia na chakras.
Chakras ni vituo 7 vya nishati kwenye mwili wa mwanadamu
kila kituo kina rangi, sauti(note ya mziki) , hisia yake na somo lake la
kiroho.
Hivyo unapobadili rangi unazojizungushia,sauti unazo
sikiliza (mfano 528 Hz), Mawazo unayoamua kushilia, unapoamua fikra zako kuwa
huru, yaani kupuuza hoja za kisiasa,
ki-mifumo ya elimu , ki dini, ambazo
hujengea watu hali ya kitu flani ni hivi na kufanya fikra zao zisifafanue jambo
wakiamini tayari limesha fafanuliwa na ELIMU,DINI,SAYANSI AU SIASA.
Toa Fahamu yako kifungoni ipe uhuru wa kujipambanua iachilie
yenyewe ina jua pa Kwenda inawajua watu wake, na watu wake wanaijua tangu siku
unazaliwa. Mambo yatakwendea kwa namna ya ajabu sana,
Kuwa mtu asie na kiburi , kuwa mtu mwenye shukrani, ili
usivamiwe na bila yeye mimi siwezi , bila yeye nisinge fika hapa, usimavamiwe
na hapa nilipo siwezi kufika pale bila mtu flani kuninyenyua.
Wewe ni sawa na mbegu ya mmea ambayo inauwezo wa kuota hata
pale jua likiiunguza sana lakini siku ikipata maji ikiwa kwenye udongo huota
kwa furaha. Kumbuka mvua inanyesha bila kujua imefurahisha vitu vingapi, acha
kuabudu msaada kuwa na shukrani peke yake ndio inatosha. Kama ambavyo mbegu
haina mdomo haijaiambia mvua inyeshe lakini inanyesha kama utaratibu wake au
jukumu lake.
Unatakiwa kutambua shali zikuzote hutaka malipo ila heri
hakuna anayeweza kuilipa na haitaki malipo. Epuka kutoa huku unasema mimi ndio
nimempa , au nimekupa kitu flani lakini unanitusi, hauniheshimu, umenikimbia,
umenisaliti wote ni moyo wa giza. Toa kama desturi , Fanya unacho kiweza
usifanye usichokiweza na wala usisicho kiweza kisikupe stress kwa maana
ungekuwa unakiweza ungekuwa na uwezo nacho timiza majukumu unayo yaweza ili
upate amani(high frequency).
Mwili hutenda kulingana na Frequency unayo ichagua wala
hauelewi maneno wala lugha yoyote hutumikia frequency ulio ipokea ndio maana
hata uchawi ni frequency ilitengenezwa kulenga mwili wako pindi unapo ungana
nayo basi inaanza kukuathiri na mwili unatumikia frequency sio maneno, au lugha
yoyote. Mtoto mwingine akikuta mama yake analia naye anaanza kulia , kwa kuwa
yeye yupo kihisia zaidi kuliko mtu mzima, kwamba mwili wake unatumikia
frequency iliyo zunguka hapo ya huzuni nayeye anajikuta analia.
Kabla hatuja endelea nitoe lai ninapo sema Malaika
usifikilie picha ya kiumbe flani , ni dhana ya kumaanisha high frequency tabaka
flani karibu na nguvu kuu tukufu takatifu ya juu kabisa.
Kwenye masomo tuliyo soma nyuma tulijifunza kwamba Malaika
wakuu, Roho za Nuru, na Mababu Wema humtembelea mtu anapokuwa kwenye High
Frequency, Pia tukasema Roho wasumbufu , mizigo ya mababu, na Nguvu za giza
huja kwenye Low Frequency.
Namna ya haraka ya kujikinga athari ya Low Frequency ni pale
unapo ziona hisia hizo za low frequency ziepuke kwa kuchagua upendo, Tafakari,
Msamaha, Shukrani au nia njema kulingana na hisia iliyo kuja. Kwa maana hizi ni
ngao zako za Frequency ya juu.
Ulimwengu wa roho unaingiliana na Mawazo yako hivyo kwa
kubadilisha frequency, unabadilisha roho unazovutia.
Katika elimu za kiroho utakutana na kauli wewe sio huyo, au
wewe sio masikini , au mwingine ataenda mbali atakwambia ramani yako ya maisha
ilichorwa kabla hata hauja zaliwa na ukiipata ramani yako basi kwenye maisha
haya utapata kufahamu ufanye kipi na kipi usifanye.
Elimu ya Unajimu wa Kale ndio iliyo leta Imani za Dini na
Sayansi za kiwango chochote unacho ona leo, watu wakale waliangalia mzunguko wa
sayari na magimba mengine angani na kuhusianisha na maisha ya viumbe duniani ,
walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutabili matukio. Elimu hiyo ya kupata majibu
kutokana na mzunguko wa sayari iliingia kwenye elimu ya unajimu.
Ebu tuangalia uhusiano wa unajimu au unajimu wako
unamaanisha nini kwenye maisha yako ??
Unajimu utakupa au utakuonyesha Frequency yako ya Asili
frequency uliyo zaliwa nayo, pia unakuonyesha uwezo wa juu (Uwezo wa Asili) ,
Karma ya zamani (Low Frequency) na
unajimu huo huo utakuonyesha eneo ambalo kwenye maisha unatakiwa kutoa mwanga ,
au huduma.
Zana ya kila mtu ana ubora wake na uzaifu wake inatoka hapa
, ni kweli kila mtu alizaliwa na uwezo wake mkubwa wa pekee(High
Frequency), na alizaliwa na uzaifu
pia(Low Frequency), na yote haya unayaona kwenye unajimu wa mtu.
Sasa ulivyo zaliwa kila sayari ilikuwa sehemu flani, kama
vile tuseme ule muda ulizaliwa sayari ilikuwa inatembea lakini ilikuwa imefika
mahali flani muda huo unazaliwa wewe , lakini kuzaliwa kwako bado yenyewe ina
endelea na safari yake tu, sasa kulingana na imefika wapi kwenye safari yake
nguvu yake huathiri maisha yako. Ndio maana utaona kuna nyakati nzuri unapitia
na mbaya zinakuja pia, ukiwa na elimu unakuwa na msimu wa kukusanya na msimu wa
kupoa kwa kuwa ukipisha na majira yako mwenyewe utakutana na hatari , hasara na
mambo yaliyo faa, hivyo kumbuka unatakiwa kuchuma na kukaa kivulini kusubili
msimu wako.
Msimu wakuchuma ukiwa haujui wala hauelewi ukapita hauja
jipanga ndio utalaumu watu mpaka ukome.
Sasa safari ya sayari angani
hukukumbusha wewe somo, hukulazimisha kuponya,hukuvuta kwenye mwanga au
giza.
Ni jukumu lako kujua ramani yako , na ufahamu wewe ndio
dereva.
Jua lilikuwa wapi wakati unazaliwa , Hapo lilipo kuwa
panahusiana na nini ?? basi wewe hapo ndio jukumu roho yako ilikuja duniani.
Ukiishi jukumu hilo hakuna uchawi wa mtu wa kukuangusha wewe , Ukiishi jukumu
hilo upo kwenye uwezo wako mkuu mababu wema , Malaika wema wanakuwa na wewe
muda wote kukuunga mkono ili jukumu litimie hapa duniani , Kuishi jukumu lako
ndio hapo husema nyota yako ina waka sana, hapo hatima yako inafunguka kabisa ,
unawaka kama taa kwenye giza nene.
Hivyo ulimwengu haukuamrishi bali unaitikia kama redio
inavyopokea kituo unachochagua, ndivyo hivyo maisha yako yanavyokujibu kulingana na ulivyo
chagua.
Ukiwa kwenye low frequency unavuta mambo hasi mfano huzuni,
watu wabaya, kukwama,magonjwa, na mambo mengine kama haya ya giza.
Ukiwa kwenye High Frequency , unavuta
fursa,afya,wingi,mahusiano mazuri, mafanikio. Frequency yako ndio dua/sala yako
halisi. Ulimwengu unasikia kile unachotuma, na si kile unachosema.
Kwa hiyo nini ufanye sasa.
Roho yako inajua cha kufanya sema umeifunga na mitazamo
mingi ya kidini,kielimu,kifamilia,kimakundi,kisiasa,kijamii. Unatakiwa kuiacha
huru ili iishi kusudi la yenyewe kuwepo hapa duniani, inajua wapi itapata
ufahamu wa kutimiza kusudi lake , inajua watu walio zaliwa kwa ajili ya
kukusaidia katika dunia ya nyama kutimiza kusudi na roho za mababu zako wema
utake usitake wapo Pamoja na wewe ili kukuongoza maana ndio wasimamizi wa ukoo
wako wewe.
Huwezi kuhusiana na ulimwengu wa kiroho kwa wema kama akili
yako ipo na mawimbi ya beta(KIFUNGO cha mitazamo mingi ya
kidini,kielimu,kifamilia,kimakundi,kisiasa,kijamii), Ufahamu wako mkuu ,
ubunifu na uwezo wa ndani yako unakuwa mubashara wakati akili ipo kwenye
mawimbi ya ALPHA,THETA na DELTA (DELTA_ndio maana watu hulazwa ili mwili
ujiponye).
Beta huzima yenyewe ukiwa umelala hata kama haujui, beta
ikizima jicho la tatu linakuwa wazi kabisa bila wewe kujua, ukiwa haufahamu
kutembea na fahamu Beta ikiwa imelala ndio una kuwa una ota mazingizonge ,
wachawi wanakuwangia watakavyo kwa kuwa malango ya kiroho yapo wazi.
Ni hatari kutokufahamu kitendo hiki cha kiroho, maana fahamu
zako huelea kama hazina mwenyewe,
Zoezi la muhimu ili kuzinduka ni ku Jifunza namna ya Kuzima
Beta, kwa utashi wako wewe ukijifunza namna ya kuzima mawimbi ya beta basi ndio kujitambua kwenyewe.
Watu wanafundisha Meditation, wengine wanafundisha kufungua
jicho la tatu, mimi nakuambia jifunze kuzima Beta , maana ikizima unakuwa
kwenye Alpha na Theta , na ukiwa kwenye Alpha na Theta jicho la tatu linakuwa
wazi bila kulazimisha.
Na vyote hivyo mazoezi ya meditation, elimu sijui ya
kujitambua, sijui mazoezi ya jicho la tatu, sijui dawa ya kutoa uchawi, sijui
kusafisha nyota, sijui kuombewa, sijui kuomba kwa yesu na mambo yoyote ya namna
hiyo, vyote hivyo hulenga kuweka kwenye utulivu wa ALPHA na THETA ili roho yako
ichukue utawala, iwe na nguvu yake , iwe na usawa wake wa asili.
Hata kupata Elimu huwa tuna elimisha BETA, ili kupata
uthibiti wa mambo kadhaa, Beta ni mawimbi yanayo funga kabisa uelewa wa ndani
ya mtu, beta ni mawimbi watu huwa wategemezi wa kifikra, beta inataka kujua
kila kitu kwenye ulimwengu wan je, hivyo yule anaye jua vitu vingi vya nje huwa
wengi wanamtegemea kwa maarifa. Mara zote BETA yako kila kitu isicho kijua,
itakwambia hauwezi hiki, wakati ukiweza kuizima akili ya fahamu itakueleza kwa
fahamu na uwezo wako halisi. Uwezo wa ndani ndio hiyo wengine wanaita kipaji au
sijui genius yaani ule uwezo wa kufanya kitu kwa ubunifu bila kujifunza
darasani.
Hizi Ni njia ninazo zipendekeza mimi kwa ajili ya kuthibiti
SHETANI WA KWENYE VITABU VYA DINI (BETA).
1.Itoe akili yako kwenye mawimbi ya beta kwa kutumia sauti
maalumu, sauti ya Nota za muziki, kila nota ina mlio wake. Ivi unajua kwanini
muziki ni burudani ?? kwa nini mziki wengine unawatolea stress ?? ivi unajua
mzuki wa mtu mwenye kipaji unadumu ?? haukinai kabisa kwa kuwa una mitetemo
iliyo tiba, wenzetu wazungu wanafahamu hili tangu zamani, ndio maana sisi kwa
ajili hautujui basi ndio sisi hujifunza kutoka huko.
Nilikwambia kuhusiana na chakras , chakra zikiwa kwenye
usawa basi mwili na roho huungana na kufanya kwa usahihi wake .
Sasa unatakiwa kuipigia kelele BETA hadi izime , ufanya
hivyo kwa kuliza sauti ya kila chakra kwa angalau dakika 3-5, mfululizo hadi
chakra zote 7 kila chakra ina nota yake.
A.liza sauti ya chakra
B.fikiria rangi ya chakra
C.kuwa mvumilivu kwa dakika tatu. Huku sauti hiyo ikilia
masikioni
Chakras frequency huwa na kipimo kwenye sauti (HZ)
| Bonyeza picha kusikiliza sauti za Frequency |
i.Mzizi (uti wa mgongo) rangi yake ni nyekundu note C(do),
frequency 262 Hz, hisia ya hapa jiambie niko salama alafu hisi usalama, huku
sauti inalia masikioni, huku unavuta picha kichwani ya rangi nyekundu.
ii.Tumbo(chini ya kitovu) rangi yake ni machungwa nota
D(re), frequency 294 Hz, hisia ya hapa ni Ubunifu,jiambie mimi naweza
kutengeneza furaha na hisia safi. Kwenye kichwa fikilia rangi ya machungwa huku
sauti ikiendelea kulindima masikioni.
Fanya hivyo kwa chakra zingine
iii.Jua (tumbo la juu) manjano, nota E (mi), frequency 330
Hz, Hisia ya hapa ni Nguvu, jiambie mimi nina nguvu kamili ya kufanya maamuzi
sahihi.
iv. Moyo (Kifua)kijani, nota F(fa) 349 Hz, hisia ya hapa ni
upendo, jiambie ninatoa na ninapokea upendo bila masharti.
v.Koo(koo) Bluu G (so) 392 Hz , hisia ya hapa ni
Ukweli, jiambie mimi husema ukweli wangu
kwa ujasiri na uwazi.
vi.Jicho la tatu (paji la uso) rangi ya Nili(Indigo) A (La)
440 au 432 Hz, hisia ya hapa ni Utambuzi , jiambie akili yangu ni wazi ninaona
maono yangu kikamilifu.
vii.Taji(Juu ya kichwa) zambalau B (si/ti) 494 Hz , Hisia ya Muunganiko, jiambie mimi nimeungana na uungu.
Chakra ziko 7, sauti ya nota ilie angalau dakika 3 hadi tano
kwahiyo ikiungana inakuwa audio yenye urefu wa dakika 21 au 35. Hata kama usipo
fanikiwa kuvuta hisia ya Langi Fanya zoezi hili kwa wiki moja. Ukiona ni ngumu
sana kuvuta picha sikiliza sauti peke
yake.
Hata kama unastress nzito kiasi gani sikiliza iyo audio
kisha lala hakika utaanza kupata maono ya mazuri, na sio maono tu kiwango cha
kuhisi na ufahamu wako utakuwa unaongezeka kila siku, uwezo wa kukumbuka ndoto
utaongezeka. Hekima itaanza kuwa kubwa sana.
Kuna muda ukilala basi ndoto zinakuja mbaya , kama unaweza
kupata mdarasini wakati unalala ile harufu yake iwe inakupiga , hata ukipitiwa
na usingizi ndoto utazifurahia sana.
Hilo ni zoezi la kuthibiti frequency.
Ili
uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia
masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili
ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu
changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na
inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.
Nimalize kwa
kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh
25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada
ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 ,
BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA
KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.
0 Comments