Jinsi mwendo wa sayari unavyo athiri maisha ya kila siku

 Leo tuunganishe maarifa ya frequency , Astrology na tabia zako za kila siku. Hapa ndipo tunaanza kuona jinsi anga “linavyoongea” na nishati yako – kila saa , kila siku na kila mwaka.

Tumeangalia kwenye somo lililopita kuwa transit ni hatua za sasa za sayari angani, na jinsi zinavyogusa frequency za sayari kwenye ramani yako ya kuzaliwa. Sasa tunazama zaidi kwenye transit za kila siku na athari zake.



Transit ya kila siku = mabadiliko ya kila siku ya Frequency, ukiachilila sayari zilizo mbali na jua sayari zilizo na mwendo mdogo ambazo huchukua muda mwingi kukamilisha mzunguko wake wa kuzunguka jua mfano (pluto, Zohali,Neptune), kuna transit ndogo zinazotokea kila siku(sayari zingine zinakimbia haraka haraka kulizunguka jua). Hizi ndizo zinazoamua mood yako, nishati, msukumo, ubunifu, na hata muono wa siku hiyo.

Kumbuka katika unajimu mwezi nao upo kwenye orodha ya sayari za unajimu. Na mwezi kama navyo fahamu unazunguka dunia kila siku kwa kasi kubwa hivyo tutaanza na athari ya mwezi.

Mwezi (Moon Transit)

Mwezi hubadilisha ishara kila siku mbili na nusu 2.5, na huu ndio unao athiri hisia zako za mara kwa mara, intuition, mood na subcoscious kwa kasi. 

Kabla sija endelea , kuna mtu aliniuliza maana ya intuition, (hii ni hisia ya ndani, fahamu ya papo hapo, au niseme uwezo wa kuhisi/kuelewa kitu haraka bila kufikiria sana au bila Ushahidi wa wazi) uwezo wa kujua au kuelewa jambo moja kwa moja kupitia hisia za ndani, bila kutumia hoja au uchambuzi wa kina.

Tuendelee sasa , kwa maana hiyo sasa transit ya mwezi ndio sababu “kuna siku unaamka ukiwa na shauku, nyingine ukiwa mpole, nyingine ukiwa na roho ya kutaka kujitenga” si kwamba ni kubadilika kusiko na sababu bali ni frequency ya mwezi imebadilika.

Lakini ukiachana na mwezi zipo sayari zingine zilizo na kasi ya kuzunguka jua, kama vile

Mercury-mawasiliano, akili,mabadiliko ya taarifa.

Venus – Mapenzi,pesa,urembo,Ladha

Mars- motisha, nguvu, msukumo na vitendo.

Basi hizi zikifanya transit ndogo, zinabeba frequency ya kukukumbusha kwamba “shughulikia eneo hili leo” kwa mfano halisi Mercury Retrograde, mercury ikirudi nyuma (retrograde), inasukuma low frequency kwenye moja mawasiliano, pili kwenye teknolojia, tatu mikakati, nne mipango. Somo lake sasa katika hayo “inasema sitisha, angalia upya,rekebisha,zungumza kwa utulivu,acha fujo (usiisikilize akili yenye mawimbi ya Beta).

Somo lijalo tutangalia na tutazungumza tena nyumba/milango 12 ya unajimu

Ili uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 

BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.


………………………………………………………………………………..

Zipo nyumba 12 au milango 12 ya unajimu hadi sasa, hizi humuonyesha kila mtu ramani ya maeneo ya kitu flani kwenye maisha, huonyesha eneo maalum la maisha ambamo frequency ya sayari husika itajidhilisha, na hapa ndio msingi wa kuelewa wapi maisha yako yanachochewa na frequency ipi?? 

Sasa hapa ni nyumba,frequency na maana yake.


Nyumba/Mlango: 1(Hamali/Kondoo) Aries

Eneo la Frequency na sayari: Mizizi(root chakra)/Mars(mirihi)

Maana: Utambulisho,mwili,tabia ya nje


Nyumba/Mlango: 2 Thauri(Ng’ombe/Taurus) 

Eneo la Frequency na sayari: Kiuno/(venus/zuhula)

Maana: Fedha, kujithamini,mali


Nyumba/Mlango: 3 Mapacha/Gemini

Eneo la Frequency na sayari: Koo/(Mercury/Zebaki)

Maana:Mawasiliano,ndugu,kusoma


Nyumba/Mlango: 4 (Saratani/Kaa)Cancer

Eneo la Frequency na sayari: Moyo/(Moon/Mwezi)

Maana: Familia,Mababu , nyumba


Nyumba/Mlango: 5 Simba/Leo

Eneo la Frequency na sayari: Utumbo/(Sun/Jua)

Maana: Ubunifu,upendo,Watoto


Nyumba/Mlango: 6 Virgo/(Mashuke/Bikira)

Eneo la Frequency na sayari: Koo/Mercury

Maana: Afya,kazi ndogo,tabia za kila siku


Nyumba/Mlango: 7 Mizani(Libra)

Eneo la Frequency na sayari: Mahusiano,ndoa,ushirika

Maana:

Nyumba/Mlango: 8 Scorpio(Nge)

Eneo la Frequency na sayari: Jicho la Tatu(grand pineal)/Pluto

Maana: Mabadiliko ya kina, fedha za wengine( urithi)


Nyumba/Mlango: 9 Mshale(Sagittarius)

Eneo la Frequency na sayari: Taji(Crown chakra)/Jupiter

Maana: Imani, falsafa,safari ndefu, upanuzi(expansion)


Nyumba/Mlango: 10 Mbuzi(Capricorn)

Eneo la Frequency na sayari: Taji(Crown chakra)/Saturn

Maana: Kazi, heshima, wajibu wa jamii


Nyumba/Mlango: 11 Ndoo(Aquarius)

Eneo la Frequency na sayari: Taji(Crown chakra)/Uranus

Maana: Malengo ya baadaye,marafiki,jamii


Nyumba/Mlango: 12 Samaki(Pisces)

Eneo la Frequency na sayari: Jicho la Tatu/Neptune

Maana:Siri,subconscious,uponyaji,karma


Unaweza usielewe hapo juu hapa nakupa ufunguo wake sasa, fahamu unapochanganya,

Sayari

Nyumba

Ishara

Unapata picha kamili ya Frequency ya eneo Fulani la maisha ebu tuangalie mfano, Mars(msukumo) kwenye Nyumba 2(fedha)-> mtu hupata msukumo wa kupambana kutengeneza pesa.

Neptune(maono) kwenye Nyumba 12 mtu ana

-- intuition kali(hii ni hisia ya ndani, fahamu ya papo hapo, au niseme uwezo wa kuhisi/kuelewa kitu haraka bila kufikiria sana au bila Ushahidi wa wazi) uwezo wa kujua au kuelewa jambo moja kwa moja kupitia hisia za ndani, bila kutumia hoja au uchambuzi wa kina,

--maono

---vipaji vya kiroho.

Somo linalo fuata tutaangalia maeneo mawili kwenye ramani yako yanayo onyesha nguvu za mababu na roho ya ukoo.

Ili uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 068

2329852 , 

BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.



Post a Comment

0 Comments