Jinsi ya kujua uwezo wako wa ndani

 Mtu asiye na ufahamu na mambo ya kiroho anaweza kupuuza, ujumbe wa kiroho ili usipuuze kwa urahisi uliza kwa watu kwamba ivi ni kweli mtu anaweza kupandisha mapepo na akaongea sauti isiyo yake?? Waulize vizuri uhalisia huo kisha njoo endelea kujifunza elimu za kiroho.

Nataka kusemaje ni kweli kunaweza kuwa na upotoshaji katika elimu za kiroho lakini ili kuelewa maarifa haya ni muhimu kuepuka fikra duni, na kujilazimisha kuto kuelewa kwa kuwa eti amna chuo cha kusomea elimu hizi unacho kifahamu zaidi ya dini. Unaweza chukua ninacho fundisha na kisha ukafanya utafiti sehemu nyingine ili kujirizisha kwa kuwa na wewe ni mtu mwenye utashi kama mimi. Huwezi kutegemea kuambiwa kila kitu lazima ushughulishe ubongo kutafuta huku na kule ili kuokoa kizazi baada ya wewe.

Wasimamizi wako wa kiroho wanaona kuliko wewe, wanajua kuliko wewe , wanaweza kukupeleka usipotaka, wanaweza kukufelisha jambo ili kukulinda, ukiwa jeuri wasimamizi wako wa kiroho hutoa athabu mfano kuumwa alafu haufi, mfano kama una ulinzi mkubwa wa kiroho , ukaenda kukaa kwenye harufu ya mambo ya giza lazima utaishiwa nguvu na ukitoka hapo unaweza kuugua hata siku tatu kwa kiburi chako cha kuona ishara na kuupuzia.

Hata ukipinga , hata ukiwa jeuri, una walinzi wa kiroho ambao ni mababu zako. Kwa kuwa wanajua wapi utapata nini , wapi uende na wapi usiende , wanaweza kukuongoza wewe ukaona ama ni Bahati mbaya au ni Bahati nzuri ukakutana na elimu yangu. Ni kwa sababu wanafahamu kuliko wewe.

Lakini mtu asie na fahamu za kiroho atatumia mifumo ya elimu kupinga viongozi wake wa kiroho, atatumia neno la mchungaji kupinga viongozi wake, atatumia elimu za kimwili kupinga viongozi wake wakiroho.

Amna Bahati mbaya wala nzuri kwenye maisha au kwenye hatua yako yoyote, ukiona hauna fahamu na mambo yako yanaenda jua unanguvu kubwa ya kiroho ulimwengu unakutii, ukiona mambo yanaenda jua upo kwenye sheria ,, yaani wewe kwenye kumi unapatia saba, au mara zingine unapata tano au mara zingine unapata sita kwenye kumi. Ukiwa unapata nne au tatu na matatizo yanakuwa mengi kutokana na kutoka kwenye reli kunatokana na kupuuza muongozo wa kiroho unaoupata , kutokana na jeuri, ukikaza Kichwa bila kuelewa kabisa basi watu wengine hufa.

Wengine hufa kwa ajili wanatakiwa kufa kwa ajili ya jambo flani na wengine hufa kutokana na ukaidi wao , na wengine huwa wasioeleweka kutokana na ukaidi wao, nawengine huwa machizi kutokana na kushupaza shingo kutokusikiliza muongozo wa viongozi wao wa kiroho kupitia ndoto, hisia za ghafla au namna yoyote wanayo jua wao maana ni wenye maarifa na kuona tusiyo yaona.

Unaweza kuwa na safari kwenye msitu mgeni kwako lakini usikose chakula, na ukakutana na msaada ukashangaa ajabu hiyo, hautapata sayansi itakayo elezea mambo mazuri flani ya kushangaza yaliyo wahi kukutokea hadi ukasema dah !!! kama mungu yupo basi amenisaidia katika hili.

Usipende kupinga au kudhalau kila jambo vingine ni ishara ya kukuonyesha hatari na vingine ni muongozo wa mafanikio yako. Kuchagua kuendelea kuwa mjinga wa elimu za kiroho ni kuwapa mzigo watakao kuja kuzaliwa kwa jina lako kwani watakuwa na mzigo mkubwa wa kurekebisha ambavyo hauvifanyi sasa hivi, unatakiwa kujitambua na kuishi kusudi lako. 

Somo la leo ni ufahamu tunaendelea kujifunza unajimu,mambo ya ukoo, karma na ramani ya mafanikio.

Tunaendelea kuchambua mizizi ya hatima ya mtu,mafanikio, na majukumu ya kiroho anayobeba mtu, sio lazima unielewe mimi sijui unaelewa vitu vya namna gani ila chukua kama ufahamu tu kwa kuwa ufahamu ni chakula cha ubongo nenda huko fanyia utafiti wa hiki ninacho zungumza kwa utashi wako mwenyewe huenda huko ukaelewa ninacho kifundisha kwa namna ingine kwa kutoa hapa.



Tunaangalia jinsi ramani ya kuzaliwa inavyojikita katika ukoo ,karma, na uwezo wa mafanikio ya maisha. Tuangalie vitu viwili vya muhimu leo

1.Uwezo wako kupitia ramani ya kuzaliwa(tarehe yako ya kuzaliwa) High Frequency uliyo zaliwa nayo ambayo haiwezi kukutoka.

2.Karma ya Familia(Deni la kulipwa au Kulipa)

3.Unafanyaje sasa kutokana na Karma

1.Tuanze na Uwezo wako ---Watu wengi hudhani kuwa unajimu “unawaambia nini cha kufanya.” Ukweli ni kwamba Unajimu haufungi hatima — unaonyesha uwezo wako wa juu (High Frequency Potential) na pia changamoto za kiroho (Low Frequency Lessons) ulizokuja kuzibadilisha.

Mfano Jua (Sun) + Nyumba ya 10 (Career/Mission)

Hivi viwili vinabeba Frequency ya kusudi la mafanikio ya roho yako:

Jua → Chanzo cha mwanga wako, kipaji kikuu, utambulisho wa kiroho.

Nyumba ya 10 → Wito wa kazi, heshima, mchango wako kwa jamii.

Mtu mwenye Jua katika Nyumba ya 10 ana Frequency ya uongozi, uwajibikaji, na kazi za hadhara. Roho yake ilichagua kujifunza kutoa mwanga kupitia mchango wa kitaaluma.

Unajimu Haukuambii “Kazi Gani,” Bali “Nishati Gani”

Ramani ya kuzaliwa inaonyesha Frequency ya huduma, ubunifu, mawasiliano, uponyaji, uongozi …na kadhalika.

Mfano wa pili:

 Ikiwa una Mercury (Zebaki) kwenye Nyumba ya 6 (Huduma/Tabia za kila siku), unabeba Frequency ya kusaidia, kushauri, kusikiliza, kuongoza kupitia maarifa

Hivyo unaweza kufanikiwa katika kazi yoyote inayoendana na Frequency ya Huruma na Huduma—si lazima jina la kazi liwe maalum.


2.Tuangazie kuhusu Karma ya Familia(Deni la kulipwa au Kulipa), Kuna muunganiko mkubwa kati ya nishati ya mababu, mifumo ya ukoo, ramani yako ya kuzaliwa

Angalia Sayari zilizopo kwenye nyumba/mlango wa 4 kwenye unajimu wako, Hapa ndipo unapogundua Karma ya Familia (Low Frequency Debts).

Nyumba ya 4 — Mizizi ya Ukoo

Nyumba ya 4 inaonyesha mazingira ya utotoni, mila, historia, na nguvu ya koo, tabia ulizorithi, majeraha ya kizazi (ancestral wounds)

Zingatia sna hili Ikiwa sayari nzito kama Saturn au Pluto ipo hapa:

--inaonyesha Low Frequency ambayo mababu hawakuponya

--mzigo ambao ukoo uliushindwa kugeuza

--jukumu lako la kiroho la kubadilisha historia ya nishati

Mfano:

 Pluto kwenye Nyumba ya 4 → ukoo wenye historia ya hofu ya njaa/usalama, migogoro ya ndani, majeraha ya kihisia, low Root Chakra Frequency

Kazi yako ya roho ni kutengeneza usalama, uthabiti, na uzima uliokosekana.


Unajimu → Unakuonyesha Wapi Kuvunja Mzunguko

Kwa kuona mahali ambapo mababu walipoteza Frequency, unaweza kutuma High Frequency (upendo, msamaha, uponyaji), kuvunja mzunguko wa vizazi, kuponya ukoo mzima kupitia mwanga wako.


3.Unafanyaje sasa kutokana na Karma ??

Ebu tuangalia Karma na Mafanikio ya maisha,

Ambayo ni Sheria ya Sababu na Athari ya Frequency**

Karma haimaanishi adhabu.

 Karma = Athari ya Frequency uliyotoa hapo awali(maisha ya kale).

Ni sheria ya “kile unachotuma, unakipokea.”

Karma Mbaya (Low Frequency Debt)

Hii inaonekana:

kwenye sehemu ngumu za ramani (hasa Nyumba ya 12)

kwenye sayari zinazobeba historia ya Low Frequency (kama Saturn au Pluto)

kwenye patterns zinazojirudia maishani

Low Frequency Debt =

 matokeo ya:

ubinafsi

uoga

kutokuwa na huruma

kukwepa majukumu

majeraha ya roho



Sasa roho inataka ubadilishe kuwa High Frequency.

Mafanikio = High Frequency Return

Ulimwengu hujibu Frequency:

Uvumilivu → Nafasi

Nidhamu → Mafanikio

Wema → Usaidizi

Uwazi → Fursa

Upendo → Muunganisho



Sayari kama Jupiter (Mwezaji) inaonyesha:

nyanja zako za bahati safi

fursa ambazo zinakufuata popote

maeneo unayoweza kung’aa kwa urahisi

Kwa hivyo Hapo ndipo Karma Nzuri (High Frequency History) inapolipika.


Usimamizi wa Frequency ndio Hatima Yako

Unajimu → ramani ya Frequency yako

Ukoo → chanzo cha Low/High Frequency za mababu

Karma → matokeo ya Frequency uliyoitoa

Wewe → msimamizi mkuu wa hatima yako

Kwa kutumia:

Alpha/Theta

Chakras

Healing Frequencies

Unajimu

… unaweza:

kubadilisha Karma

kuponya ukoo wako

kuondoa vizuizi vya zamani

kutengeneza njia ya mafanikio ya kiroho na kimwili

Roho yako ilichagua majaribu fulani ili uangaze zaidi.

 Una uwezo wa kubadilisha Low Frequency kuwa Nuru.

 Hiyo ndiyo ramani ya mafanikio ya kweli.



Ili uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 

BASI

 UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.


…………………………………………………………………………..


Post a Comment

0 Comments