Tofauti kati ya Malaika na mababu katika mawimbi

 “A” | Malaika na mababu, mtu utawezaje kutofautisha sauti za mababu na sauti za Malaika?? Katika sura ya tatu ya kitabu changu Cha MITETEMO YA KIROHO na jifunza mipaka ya kimawimbi, kwenye safari ya kiroho, jambo kubwa linalowachanganya watu wengi unakuta ana maswali “hii sauti ninayoisikia ni ya nani?? Au Ndoto hii nimetumiwa na nani ?? je ni ujumbe wa kiroho au ni Mawazo yang utu ?? “ sasa unatakiwa kutambua ulimwengu wa kiroho hauzungumzi kwa sauti za mdomo kama sisi; ulimwengu wa kiroho unazungumza kwa frequency , na si kila hisia , maono au sauti inayokuja wakati wa ndoto au tafakari inatoka kwa chanzo kikuu(MUNGU). Baadhi hutoka kwa Malaika, zingine hutoka kwa Mababu, na nyingine hutoka kwa mizigo ya kifamilia isiyoisha. 

Kuelewa chanzo cha ujumbe ndiyo msingi wa usalama wa kiroho, ukielewa unachokipokea utajua kama ukikubali, ukitafsiri au kukikataa. 

Kuna vyanzo viwili vikuu vya ujumbe wa kiroho, na unatakiwa kuelewa kwamba ulimwengu una tabaka za frequency. Na kila tabaka lina wakazi wake, wenye lengo lao. 

Kwanza ni tabaka la High Frequency – Hapa ndipo huishi Malaika,Viongozi wa kiroho na mababu wema.

Pili kuna tabaka la Low Frequency – hapa ndipo wanaishi roho zilizobeba hasira,Mawazo(stress),majuto au zigo waliloondoka nalo duniani. 

Hivyo kabla ya kutafsiri ujumbe, lazima ujue unatokea wapi kimawimbi, High frequency inabeba upendo,amani,uwazi,mwanga. Low Frequency inabeba hofu, mashinikizo, haraka,lawama, au kutishia.

Tofauti kati ya Malaika na mababu katika mawimbi, 


Malaika na viongozi wa kiroho wanaishi mbali zaidi kimwanga. Wenyewe wanakupeleka juu, wanakufanya ujione huru, hawakuongezei mzigo, hawakuongezi presha na wala hawakuongezi hofu. Ujumbe wao hupitia kwenye moyo, si kwenye wasiwasi , unapo usikia unahisi usalama mkubwa ndani ya moyo wako, hata kama ni ujumbe wenye onyo.

Mababu ni wa karibu zaidi na damu yako. Wao wanajua historia ya familia, wanaelewa majeraha ya vizazi, na mara nyingi ujumbe wao unakuja kwa njia ya maisha ya kawaida kama ndoto,hisia nzito au Mawazo yanayorudiwa(kuwa makini na hisia zinazo kurudia rudia)

Lakini kitu kimoja cha muhimu sana kuna mababu wema ambao ni kama walinzi waroho, ujumbe wao nim wanga, onyo la upole, na faraja. 

Lakini pia kuna mababu wasumbufu, ni roho za mababu ambao wapo kwenye low frequency walizo kufa nazo. Ujumbe wao huwa na hisia ya uzito, hofu, au lawama. Mara nyingi wanakuwa wanatafuta msaada kwa walio hai ili roho zao zipande kwenye frequency za juu na wala si kwa sababu wao wana nguvu ya kiroho juu yako.

Kabla hauja angalia ujumbe wenyewe wa kiroho, iwe ni kwenye ndoto au halisia lazima uangalie hisia iliyokuja kwako kwanza.

Tambua high frequency inakuja kama, amani,utulivu,uzito unaoinua sio ule unaokandamiza, mwanga wa maarifa, nguvu ya matumaini, mwelekeo wa kukua.

Wakati Low Frequecy huja kama , hofu nzito, presha ya haraka(Jaziba), lawama au hukumu(tabia ya kujinyonga,ulevi wa msongo wa mawazo, ubakaji,kuuwa kwenye ukoo flani hutokana na hii), mzigo wa kihisia, hisia ya kutishiwa, machafuko ya Mawazo.

Hivyo kuwa makini ukiona ujumbe unakuacha na hofu nzito , au mzigo tambua mara moja Huo si mwongozo wa Malaika au Mababu wema. Inaweza kuwa mababu wenye mizigo au sauti ya akili yako mwenyewe yenye majeraha.

Katika somo linalo kuja tutajifunza ni wakati gani ujumbe wa high frequency ( ujumbe mzuri) unakuja na niwakati gani ujumbe wa low frequency unakuja.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 

BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.


Endelea na sehemu B


“B” (Ulinzi wa Frequency)| Malaika na mababu, ni hali au wakati gani ujumbe mzuri(high frequency ) au ujumbe mbaya(low frequency ) unaingia? 

Ujumbe mzuri huja wakati wa utulivu. Wakati ambao akili ipo kwenye mawimbi ya Alpha au Theta katika hali ya mwanga wa ndani wa kiroho, tahajudi au ndoto safi. Ukiwa kwenye Alpha au Theta ndipo channel ya high frequency hufunguka yenyewe.

Ujumbe mbaya mara nyingi huingia wakati wa Beta- wakati wa stress, Mawazo ya kupita kiasi, msongo au hisia mbaya zinazo kushusha chini.

Tambua kwamba Low frequency hupenda machafuko ya akili( huu ndio wakati ambao uchawi unaweza kukupata, jinni), na High Frequency hupendelea utulivu ( hapa ndio hekima huja na uchawi haukupati) na sasa ukiona ujumbe (hisia) imeingia wakati akili ina makelele(haijatulia) kuwa makini sana.

Sasa nikupe kanuni ambayo uikumbuke ili kutambua chanzo cha ujumbe 

Chanzo cha mwanga(ujumbe mzuri) hakilazimishi

Chanzo cha mzigo(ujumbe mbaya) kinalazimisha.

Malaika au mababu wema , watakwambia “ chagua kilicho sahihi. Wanakuonyesha amani iko upande huu.”

Mababu wenye mizigo (wanakulazimisha) ujumbe unakuwa unasema “ ukiacha kufanya hivi, utalaaniwa. Lazima ulipe deni la familia.” Hivyo elewa kuwa mababu wenye mizigo huamsha mkandamizo wa vizazi.

Kwa kufanya hivi unaweza kuweka mazingira ya kupokea ujumbe mzuri , kwanza tambua hakuna njia ya mkato ya kupokea high frequency kama moyo haujatulia(ndio maana watu huvuta pumza kabla ya kuamua jambo, au ya kusema au kwenye mazoezi ya meditation). Moyo ndio chungu kikuu cha kiroho , ujumbe wowote unaopita kwenye moyo, moyo ambao haufanyi kazi vizuri, basi moyo huo utajichanganya tu. Kwa hiyo hatua ya kwanza ni kuinua frequency ya moyo (chakra ya moyo) na unawezaje kufanya hivyo ?? fanya tafakari ya rangi ya kijani au pinki, ama tumia nia ya msamaha waza msamaha jenga picha ya msamaha, ama sikiliza ya nota F ya muziki (639 Hz), ama Fanya tendo la kuacha hasira za zamani. Kwa kufanya hivyo unakuwa mpokeaji wa mwanga(utulivu) na si wa Kelele.

Kufungua moyo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kujiandaa kupokea ujumbe mzuri, lakini hatua ya pili ni jicho lako la tatu, unatakiwa ubongo wako uwe kwenye mawimbi ya Theta, kwa kuwa bila Theta Frequency huwezi kutambua tofauti kati ya ujumbe unaokuinua na ujumbe unaokutisha.

Hatua ya mwisho sasa ni thibitisha umepokea ujumbe wa high frequency ?? ujumbe wa high frequency hauhitaji kuwa na haraka kabisa. Unaweza kuja hisia moyoni, katika akili ya kawaida au katika matukio ya nje.

Sasa nikufundishe namna ya kujilinda zidi ya frequency ya mababu wasumbufu wa ukoo au kizazi chako. Kama unavyo fahamu sio kila babu ni nuru(mwanga). Wengine bado wamefungwa na historia ya familia, hasira,vitalu vya mabaya,majeraha, au uchungu, na hawa huleta maono ya ukomo (Mawazo ya kwenye familia yetu hakuna tajili),uzito, au hofu ya kurudia makosa waliyofanya. Sasa njia ya kujilinda sio kupigana nao bali ni kurekebisha frequency yao. Tumia sacra frequency hii inahusiana na kupandisha nishati ya chakra ya tumbo ikae kwenye usawa haza tumia sauti ya mlio wa nota D 417Hz, kuvunja mifumo ya vizazi, Fanya msamaha kama Zawadi ya kuwapandisha kimwanga, kata mazoea ya hofu waliyokuwa nayo(tambika),acha mtazamo wa tulivyo zaliwa ndivyo tulivyo. 

Unapo vunja Low Frequency ya familia mababu wasumbufu wanapoteza uwezo wa kukudai.

Vile vile unatakiwa kutambua mahali pa kila sauti, ulimwengu wa kiroho una utaratibu wake, kila sauti ina chanzo. Kila chanzo kina Frequency yake. Ukiwa na hofu jua upo kwenye low frequency (muda wowote utaungana na viumbe wabaya) , ukiwa na utulivu jua upo kwenye high frequency na hapo Malaika hutoa mwanga na mababu wema hutoa hekima. Mababu wenye mizigo(wasumbufu) hutoa majeraha ya zamani.

Lakini wewe ndiye unaochagua channel ya unayo jiskia. Ukiinua frequency yako channel ya juu hufunguka. Ukitesa moyo wako, Channel ya chini ndio inapata nafasi.

Jukumu lako ni moja tu kuchagua heri , na usiruhusu shali zikufuate na zikuendeshe. 


Soma linalo fuata kwenye sura ya 4 ya kitabu tutajifunza frequency ya asili ya dunia, sadaka na siri za tamaduni mbalimbali.

Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 

BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKI

WA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.



Post a Comment

0 Comments