Unajimu na maisha ya familia

Uhalisia wa maisha hutupa maswali mengi, kwenye maisha tunasikia mengi sana, jamii imekosa msaada kwa kutokutambua asili, ninaposema asili simaanishi uganga wa kienyeji au mitishamba pekee, asili na maanisha chimbuko la maisha halisi nini hasa kipo nyuma ya maisha ya mwanadamu. Watu wengi kwenye jamii wanakata tamaa ya kuishi na kujiingiza 
Jasmine 

Rosemary 

kwenye mambo yasiyo faa, wakijiambia maisha ndio haya haya. 
Mtu akiambiwa jambo flani linaleta pesa basi analikimbilia haraka sana. Ni kweli wapo watu walio fanikiwa kihalali kabisa wapo watu wenye maisha mazuri mema. Lakini tukubaliane kuna watu sio kwamba hawana akili , sio kwamba niwana mapungufu flani Hapana bali hata wao wenyewe hawajui matatizo yao chanzo ni nini. 
Muda mwingine matapeli wanafaidika, sio kwa sababu wanaowatapeli ni wajinga , ila kwa sababu mtu ni kweli anashida na hajui imemkamataje ukisha taja suluhisho basi anaona wewe ndio mwokozi wake.
Kabla sijaendelea nakumbuka nilifundisha kuhusu frequency, nikasema kuna hisia za high frequency na low frequency. Ni vitu ambavyo mtu unatakiwa kufahamu kabla ya kutumia tiba asili na mitishamba, sina maana ukitumia tiba hizo ukiwa haujui hazifanyi kazi Hapana tiba hufanya inacho Fanya muda wowote popote na kwa mtu yoyote.
Mwanadamu ameumbwa chini ya sheria za frequency na nikiumbe cha ajabu sana katika uumbaji kwani anaweza kuwa kwenye frequency yoyote anayoitaka. 
Kitu kikubwa ninacho taka kusema ni namna ambavyo unaweza tekwa na frequency bila wewe kujua. Chukulia mfano wa kutafuta channel flani ya redio mfano TBC FM utaipata kwenye frequency ya 87.9 hapo ndio utapata matangazo ya redio TBC, ukitoka kwenye hayo masafa ya 87.9 fm huwezi kupata matangazo ya Redio TBC. Vile vile Mfano radio Clouds unaipata kwenye masafa ya 100.1, ukiwa kwenye masafa hayo utasikia matangazo ya redio Clouds na ukitoka kwenye Masafa hayo huwezi kuskia matangazo ya Clouds.
Neno mambo ya giza ni sawa na kusema low frequency au kusema shetani katika elimu za kiroho. Kwa maana katika kila tabaka la frequency kuna hali zake na viumbe wake. Kwenye low frequency kuna hali zake ambazo viumbe wake huambatana nazo mfano ukatili,kutisha,wasiwasi, hofu, dhulma,masikini,tamaa,kuogopa hadi kutetemeka bila sababu, chuki, wivu, fujo, ukorofi wa viwango vyote,lawama, visasi, hatia, kujihukumu,majini, mababu wakorofi au wale ambao walikufa na hali moja wapo kati ya hizo na mambo kibao yanamna hii.
Sasa unapo kuwa kwenye moja ya hali hizo unakuwa kwenye masafa ya ulimwengu wa giza, hivyo muda huo unaweza kuungana na viumbe waishio kwenye masafa ya giza kwa kiwango hicho hicho ulicho wewe. Na roho zinazo weza kukuvaa kwa urahisi ni roho waishio huko gizani wa familia na ukoo wenu , na tabia yao kuu wakisha ungana na wewe wataka uwe walivyo kuwa wao kwa maana ndio frequency waliyo enda nayo kama alikufa na kisasi ,, ukawa unajiskia kisasi basi anakuja na anakushinikiza kiasi unaona kisasi ni halali kabisa. Kama tamaa za mapenzi zilimuua basi anakushinikiza tamaa izo izo ndio uzifanye muda huo . unaweza kuwa shahidi watu wengi akisha fanya tukio la kushangaza baada ya muda na yeye mwenyewe anakuwa anaogopa anashangaa, kutokana wakati anafanya hivyo alikuwa amevamiwa.
Sasa frequency hizi mbaya pia zipo za kutengenezwa, watu wanatumia nishati za ulimwengu kuzalisha low frequency za viwango wanavyo taka wao, sasa elimu hii ya kuzalisha low frequency ndio huo Uchawi Mweusi, 
Uchawi Mweusi umejaa shali shali , mali za mikataba, umasikini , ukatili wa kumwaga damu. 
Lakini kitendo cha kuzalisha high frequency ni uponyaji na ufunguaji wa hatima za mtu zile alizo zaliwa nazo, mafanikio ya halali yanatokana na uwezo wa mtu alio zaliwa nao. Unaposikia kufungua riziki , ni uwezo wa kubaki kwenye high frequency kwa muda mrefu , kitu kinacho Fanya vipawa na uwezo wako ufanye kazi kama ilivyo kusudiwa wakati unazaliwa. Kwa hiyo kinacho kufanikisha sio dawa ni wewe mwenyewe. Nguvu ulio zaliwa nayo kuna viumbe wapo wanaweza kuitii , hata watu ndio huo wanaita mvuto, ndio maana wataalamu wadawa za asili wanasema wakusafishe ndio wakufanyie dawa ya mvuto. 
Uchawi Mweupe , ni upendo, shukrani, ujasiri, amani, utulivu, haki, furaha,hekima, ulinzi vyote hivi bila masharti yoyote ni uchawi mweupe wa mungu (Chanzo Kikuu) hakuna masharti yoyote, ndio maana mnayama akifanyiwa dua ya nia njema kabisa hutii na anakuwa mpole kwa ajili ya kuchinjwa anakufa akiwa na amani kabisa kwa kuwa ana roho inaishi kwenye sheria ule uhai wake mnyama anakupa bila masharti yoyote.
Ili kuzalisha low frequency watu hutumia nishati za low frequency mfano miti flani ambayo kwa asili ina low frequency mfano mkonge, mkwaju,mvule,mjoholo wa porini,foxglove,kichaa cha mbwa pori,datura. Hata sumu maarufu kali(za kisasa) hutengenezwa na miti ya low frequency kwa kiasi kikubwa.
Ili kuzalisha high frequency ukiacha nia njema na wema miti inaweza kulazimisha high frequency iwepo kwa kuwa ina nguvu hizo miti mfano kivumbasi,mdarasini,ginseng,pine,karafuu,jasmine,rosemary(dawa ya kienyeji ya sulua hii), Mint(nanasi pori),Sage ya Afrika,lavender , mchai,mzaituni,sandalwood,mwarobaini mweupe.

Kwenye kitabu changu nimeorodhesha miti mingi zaidi.
Somo lilikuwa ni jinsi frequency inavyo kukamata bila wewe kujua , nimewahi kukwambia jiepushe na hali za low frequency kwa maana huko huishi viumbe usio weza kuwaona wanaingiliana na wewe kwa hisia na kukupelekea hali mbaya zaidi, hivyo epuka hali za low frequency kwa gharama yoyote kwa maana hata uchawi utakudaka kama kuna mtu alikuloga hata miaka mingi imepita ukiwa kwenye hali hiyo lazima utakuendesha kadili muda, hatakama sio uchawi watakuja majini au mababu wa familia yako walio kufa na low frequency. 
Wakati mwingine unaweza ukawa mgumu kuingilika zikatumika mazingira yanayo kuzunguka mfano mtu atakuja anakufokea anataka akuambukize hasira, usikubali , mtu atakuja anakuhuzunisha usikubali kuhuzunika , mtu atakuja anakukumbusha fikra mbaya usikubali,, 
Sio kila mtu anaye kuja kukuletea hali hizo ni mbaya Hapana huenda yeye mwenyewe hana elimu hii hivyo ameathirika na izo low frequency na zinamwendesha , wala hajui , unaweza ukamweleza jambo mara anaanza kukukatisha tamaa. Kukuambia hiyo haiwezekani kabisha wakati unaona unacho kiwaza sio ubaya .
Kuna muda huwaita ndugu au marafiki wanawaloga, kwa kuwa hao watu hawana elimu ya kiroho na wao wameathirika na hawajui, asije kukuambia mtu mzazi anakuloga ukaamini kirahisi, tambua mzazi ni mtangulizi wako kama hana elimu hii na yeye hajui , chochote hasa wazee wengi wame kua wakati wa ukoloni elimu hawana kabisa kwa hiyo roho wa ukoo wanakuwa wanakufikia wewe kupitia yeye. Mfano unakuta mzazi hataki ufanikiwe, hataki upate kazi kwa sababu yeye hakufanikiwa hataki ufanikiwe anataka uwe kama yeye tu, hapo sio yeye na yeye ni mwathirika wewe kuwa msiri na mambo yako na kuwa na furaha na wazazi , ndugu na jamaa zako. Shukuru umeumbwa na umetambua elimu hii kubwa sana.
Nina mengi sana ya kunena na wewe ila andiko litakuwa refu sana. Ninacho weza kusema unapo jitambua ni rahisi kuufikia utajili kwa halaka maana utajili au pesa zinafanya mtu atatue matatizo nimekwambia matatizo ni low frequency na pesa zinatatua matatizo kwa hiyo ni high frequency ya tabaka unalotakiwa kulifikia na kulivuka kwani ukifika uka ganda zitakuendesha zitakufanya uzi abudu , kitu chochote kinakufanya ujiskie amani furaha isiyo na masharti ni hali ya mungu(Nguvu kuu tukufu takatifu) hiyo.
Usipuuze kila kitu kilichopo kwenye vitabu vya dini , vitabu vile vina mafumbo ya ufahamu wa juu kabisa ambao mtu unaweza kuufikia kwa kuishi sheria za frequency.
Baada ya kunena hayo leo kutoka kwenye kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO nilipanga tuangalie unajimu na maisha ya familia. 
Kwenye kitabu nimesema kwamba Kila mtu wa familia yenu ana ramani yake ya kuzaliwa na Frequency yake. Lakini kuna maeneo mawili muhimu yanayoonyesha * nguvu za mababu na roho ya ukoo*:

Nyumba ya 4 — Frequency ya Mababu
Hapa ndipo:
-siri za kizazi
-tabia mlizorithi
-patterns za familia
-nishati ya mama/baba
 hujitokeza.
Sayari ikikaa hapa, inaonyesha mzigo au baraka uliyopewa.

Nyumba ya 12 — Frequency ya Karmic Debts
Hii ni nyumba ya:
-mambo yaliyofichwa
-majeraha ya kiroho
-karma za maisha yaliyopita
-vipawa vya kiroho
-uponyaji wa mwisho
Sayari zenye nguvu hapa huonyesha “mizigo ya roho” unayokuja kushughulikia ili upate mwanga.
Mfano wa Kufundishia
Mfano muhimu: Ikiwa Saturn (sayari ya Low Frequency ya nidhamu, mipaka, changamoto) ipo kwenye House 2:
Inamaanisha:
-changamoto zako za kiroho zinahusu fedha na kujithamini
-ukosefu wa nidhamu unaweza kushusha Frequency
-transit za Saturn zikija, zinakuambia:“Jenga misingi. Fanyia kazi nidhamu ya kifedha. Punguza matumizi ya Low Frequency.”
Sayari yoyote inapofanya transit juu ya nyumba fulani, inasimama kama mwalimu, ikisema: “Hapa ndipo unapopaswa kuweka Alpha/Theta yako sasa.” Alpha/Theta ni mawimbi ya ubongo nilifundisha hata youtube ipo.
Houses(Milango ya unajimu) ni kama kioo cha maeneo 12 ya maisha yako.
 Sayari ni chanzo cha Frequency.
 Transit ni taarifa ya kimungu ya hatua.
Kwa kutumia:
-Alpha/Theta(mawimbi ya ubongo uliotulia kabisa)
-Chakras( vituo vya nishati kwenye mwili wa binadamu)
-Astrology
… unaweza kuelewa kwa usahihi ni wapi pa kuweka umakini ili kuinua Frequency yako na kukamilisha kusudi lako la maisha.
Ili uelewe jambo vizuri ni muhimu kulitafakari mara kwa mara. Kitendo cha kupitia masomo yangu mara moja moja hautapata nafasi ya kuunganisha nadhalia hizi ili ziweze kukusaidia katika maisha yako na ndio maana nakusihi uwe na kitabu changu cha mitetemo ya kiroho kwa maana kina kila kitu kwa mpangilio mzuri na inakuwa kama kumbukumbu na chanzo cha elimu kwa wanao kuzunguka.
Nimalize kwa kuku alika kununua kitabu changu cha MITETEMO YA KIROHO chenye gharama ya Tsh 25,000/= , kitabu ni nakala laini(eBook) unakipata kwenye Whatsapp yako baada ya kufanya malipo kwenye Namba 0682329852 , 
BASI UMEBARIKIWA KWA KUFANIKIWA KUPATA ELIMU HII KUBWA YA KIROHO.



Post a Comment

0 Comments