Watu wa zamani

 




Vitabu vya dini ni maandiko yanayo fundisha elimu au maarifa ya kiroho, maandiko haya siyo ya kuzuka au kutungwa bali yana chanzo chake.


Zamani za kale watu pamoja na mambo yote walifanikiwa kutunza mafundisho na maadili ya kiroho kwa namna nyingi kama vile simulizi na hata maandiko.


Watu wa zamani walielewa kuwa ulimwengu upo na kanuni na sheria katika mambo mbalimbali. Wakaelewa matatizo yanayo tokana na ukiukwaji wa sheria, wakaelewa ili matatizo hayo waliyokuwa na uhakika kwamba yanatokana na uhalibifu wa maadili na uvunjaji wa sheria, ili yasiwepo ni lazima kufuata maadili na sheria flani.

Jambo hilo likawa sababu kubwa ya kutunza maadili na sheria pamoja na maelekezo ya maadili na sheria hizo.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Kubadilishana maarifa ni jambo la asili kabisa ambalo linatokea kulingana na mazingira au hali iliyopo. Mtu mmoja anaweza akawa na ufahamu wa jambo flani, ikawa ni hiari yake kusema au kuto kusema, lakini mtu huyu mwenye kufahamu jambo flani pindi yeye mwenyewe anapo ona jambo hili linafaa kuwa wazi au yakawepo mazingira yanayo mlazimisha mtu huyu mwenye kufahamu kusema au kutumia ujuzi alionao kwa maarifa aliyo nayo kwa ajili ya kuokoa au kusaidia jambo flani.


Baada ya kusema au kutumia ujuzi wake mbele ya wengine, na ikiwa miongoni mwa hao wengine walio shuhudia ujuzi watavutiwa na ujuzi au maarifa hayo wanaweza hata kutamani kuwa na maarifa ya namna hiyo, basi kubadilishana maarifa kunaweza kufanyika kulingana na jinsi wanavyo weza kukubaliana wenyewe.


Basi sasa kila mmoja anaweza kutunza maarifa na ujuzi kwa jinsi na namna anayo ona inafaa, kwa ajili ya watu atakaoona yeye yakuwa wanafaa kujifunza kwa majira na wakati wowote wa maisha.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Kurizika ni hali ambayo ni binafsi sana kwa maana kilicho rizika au aliye rizika ndiye pekee anaweza kuelewa kwa undani namna iyo hali ya kurizika ilivyo kwake.


Kila kitu au mtu anaweza kurizika kwa namna yake yeye, na baada ya hapo anapata utulivu anao utaka yeye mwenyewe. 

Kinyume cha utulivu ni mahangaiko au masumbuko au mashaka au wasiwasi au hofu.

Watu huangaikia utulivu wao hata vitu vingine huangaikia utulivu.


Utulivu ni hitaji la vitu vingi katika uwepo huu na sio mtu peke yake na kila kitu kina utulivu wake chenyewe kulingana na kilivyo hivyo hivyo hata mtu.


Basi pia kila kitu ni cha thamani kwa kitu kinacho kihitaji.

Muda mwingine mtu anaweza kuwa na kitu cha thamani kwake lakini asielewe kama ni cha thamani kwake kwa sababu hana elimu nacho jinsi kinavyo weza kumpa utulivu wa thamani wa aina flani.


Watu wa zamani walipo elewa haya wakaona umuhimu wa kugundua kutafuta na kutunza elimu au maarifa ya jinsi na namna mbalimbali.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Watu wa zamani walijifanyia hazina za vitu vya thamani kwao wenyewe.

Ndani ya hazina zao palikuwepo na thamani za aina mbalimbali ikiwemo elimu au maarifa ya kimaandiko, michoro , alama na vitu vingine.


Maandiko, michoro na alama vilikuwa ni maelekezo ya uhalisia wa jambo flani.

Hata sasa ni wazi kuwa unaweza kusimulia au kusimuliwa jambo flani lakini usielewe namna za ndani za uhalisia wake mpaka kudhihilika kwake hilo jambo.


Pamoja na mambo yote, maandiko mengine au ujuzi mwingine ulionekana chanzo chake kuwa ni ajabu kwa watu hasa wale walio kuwa hawafahamu usomi wa elimu na maarifa ya kale hiyo na hata sasa.


Kama ambavyo hata sasa unaweza kuwa na kitu na usielewe kama unaweza fanya hivi na hivi ikawa hivi, lakini akija mtu au kitu chenyewe au mtu mwenyewe kwa hiari yake akakueleza au hata kwa kumuomba na kweli ikawa katika uhalisia kwa jinsi na namna ya maelekezo yake basi mtu unaamini na kukiishi kitu hicho ikiwa kina manufaa kwako.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Maendeleo ni utaratibu au matokeo mapya zaidi ya jambo lililokuwepo.


Kitu kinaweza kuwa hitaji lako kwa ajili ya kufanikisha utulivu flani, kika kufanikishia utulivu huo kila wakati na ukajua ndio hivyo hivyo jinsi ilivyo kumbe kuna zaidi ya hivyo usiyo ijua wewe.

Mtu anaweza kuishi karibu na mawe ambayo ni madini ya thamani kwa jambo flani na asijue kama mawe ya karibu yake hayo ni thamani kwa jambo flani, yeye akachukua na kuweka kama mapambo katika mazingira yake akijua na kufahamu kwamba ndio kinacho yastahili mawe hayo.


Mtu huyo mwenye kuishi karibu na mawe akaja kutembelewa na mtu ambaye ni wa kiroho katika makazi yake hayo na amwambie habari ya mawe yaliyo karibu naye kuwa mawe haya ni mamlaka za kiroho, zilipo mamlaka hizi roho wa machafuko , malazi na mambo flani hawawezi kabisa kusogea, na mamlaka hiyo ndio inayofanya familia iwe na afya njema, mifugo izaliane na mambo mengine.


Lakini pia aje mtu wa mambo ya teknolojia hapo kwenye makazi ya mtu mwenye kuishi karibu na mawe na amwambie mawe haya ni hodari sana kwenye mawasiliano kwa namna hii na hii.


Basi mtu huyo mwenye kuishi karibu na mawe hayo kuanzia hapo baada ya maarifa kuhusu mawe anayo ishi karibu nayo, atachukulia mawe hayo tofauti na siku zingine zilizo pita na atakuwa ameendelea katika maarifa juu ya hayo mawe.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Ni kweli kwamba kukielewa kitu vizuri sio lazima uwe umekitengeneza au kukiumba wewe, bali hata kwa kukifuatilia jinsi na namna ya utendaji wake, au kitu hiko kiku simulie namna yake au ubahatike kufundishwa na kitu kingine cha karibu yake na iko unacho jaribu kukielewa.


Basi maarifa ya kufahamu mambo yanafahamika na vyenye kufahamu pekee na sio kila kitu kinaweza kufahamu mambo yote labda kwa namna inayotakiwa ili kukidhi kufahamu.


Zamani watu walielewa kuwepo kwa uwili waka elimika na kuelimishana juu ya uwili, wakatambua kuwa kila kitu kipo katika uwili. Wakatazama kwenye maisha bayana na kuona uwili huo katika mambo mengi sana kama vile usiku na mchana, kushoto na kulia, chini na juu, wema na ubaya, chanya na hasi, mizizi na matawi, giza na mwanga.


Wakaelewa uhusiano wa sehemu mbili za uwili na hivyo wakaheshimu sheria ya uwili, kutokana na machafuko , maafa na matatizo yasiyo faa pindi mtu au kikundi cha watu wanapo kiuka sheria hii au kujaribu kutenganisha uhusiano wa sehemu mbili za uwili.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Katika uwili watu wa zamani walitambua kua kama kuna vitu vinavyo onekana basi vipo vitu visivyo onekana, wakasema ikiwa kwenye mwanga ni sehemu ya vitu kuonekana basi ni sehemu ya maisha kwa vitu kuonekana na kwenye giza ni sehemu ambayo hata kama kuna vilivyopo havionekani kabisa kwa macho ya nyama kutokana na giza na maisha hayo yanabakia kuwa siri kwa bayana ya macho ya nyama.


Watu wa zamani wakaendelea kuthibitisha uwili katika mimea. Wakaona sehemu ya matawi huonekana dhahili lakini sehemu ya mizizi ipo ardhini pasipo onekana na uhusiano wa namna hiyo ukafanya uhai wa mmea kila sehemu ikiwa na majukumu yake.


Wakaona hata mbegu ili iote na kustawi kwa usahihi inafunikwa na udongo gizani huko inaanza na mizizi kisha sehemu ya pili matawi.


Watu wa zamani wakaenda mbali wakaona mtoto hadi kuzaliwa na mama yake anaanza kutengenezwa gizani kwenye tumbo la uzazi la mama kwa muda na wakati maalumu.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Kwenye uwili sehemu moja iko na miundombinu au taratibu za siri sana zinazo fanya kuwepo kwa sehemu nyingine.


Watu wa zamani waka chukua mifano miwili mmoja wakaangalia jinsi mti ikiwa utalazimishwa mizizi ionekane bayana na macho unavyo poteza uhai wake, wa pili wakaangalia jinsi mimba inavyo tengenezwa ndani na jinsi ikiwa mtu atakata tumbo ili kuona inavyo weza kuwa hatari kwa mama na mtoto aliye ndani hata kupoteza uhai.


Basi wakaheshimu sana uhusiano mkubwa uliopo baina ya sehemu mbili za sheria ya uwili.


Wakaelewa kuwa katika uwili kila sehemu ina mambo yake na mambo ya sehemu yoyote yanaweza yasitambuane moja kwa moja isipo kuwa kwa utaratibu maalumu sana.


Sehemu moja ya uwili wakaona ni bayana kabisa na sehemu nyingine ya uwili wakaona ni sirini, watu wa zamani wakaendelea kusema sirini ndio sehemu yenye mambo mengi sana yanayo fanya uwepo na umilele wa bayana, na hivyo sirini ndio chanzo mama cha elimu na maarifa yaliyo hifadhiwa kwenye hazina za watu wa kale.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Moja ya maarifa ya siri ya zamani za kale ilikuwa ni sehemu moja katika uwili ina maarifa juu ya sehemu ingine lakini haiwezi kufanya moja kwa moja.


Hivyo watu wa zamani wakajifunza Maarifa ya kuungana na sehemu ya siri ili kupata elimu juu ya mambo mengi na iwe fahari na msaada katika maisha ya sehemu yao.


Kilicho kuwepo ni kwamba watu walijua kuwasiliana na mambo ya sirini yaani viumbe wa huko ili kupata uelewa zaidi.


Taaluma ya mawasiliano na viumbe wa upande wa pili ilikuwa taaluma ya siri zaidi kuliko zingine zozote kutokana na mtu akiweza zoezi hilo alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya na kuwa kwa namna nyingi kufuata maelekezo ya kiumbe wa sirini.


Watu wakajifunza taratibu na mambo mengi ya kujenga na ya kubomoa, wengine wakafanya siri na urithi kwa vizazi vyao.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Elimu ya utawala jinsi ya kutawala ni maarifa ya moja kwa moja kutokana na uhusiano wa sehemu mbili za uwili.

Elimu ya familia, ukoo, jamii, eneo kubwa na mambo mengine mengi.

Hivyo zamani pakawa na mambo ya ngazi za familia, ukoo, jamii na eneo kubwa. 

Hata hazina zikawa namna hiyo hiyo kingazi.


Maarifa yakaenea huku na kule, kule na huku watu wakaweka kumbukumbu na kuzifanya hazina na mali ambazo waliweza hata kurithisha vizazi na vizazi vyao.


Utawala wa eneo kubwa zilikuwa ni falme, ufalme ulimiliki vitu vingi pamoja na maarifa, lakini familia zilimiliki juzi flani ambazo zilikuwa kama haki kwao.


Hata hivyo mamlaka za sirini na mamlaka bayana ziliheshimika, sio mamlaka peke yake bali hata sheria na kanuni zinavyo fanya uwepo na umilele wa uwepo, sheria zikahukumu makosa sheria pia zika hukumu wema au mambo mema.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Kabla mtu yoyote haja anza kujadili habari ya uwepo wa dini ni muhimu atambue kuwa dini inaongelea mambo ya kiroho.


Kiroho ni mambo ya sirini, kulingana na habari za watu wa kale sirini ndio pakwanza kisha ndio bayana inafuata.


Kiroho ni habari ambayo ndio hiyo inahusisha nguvu za kiroho kwa maana ya nguvu zisizo onekana na macho ya nyama ambazo ni dhahiri zinatenda.


Kuachana na watu wa kale mambo ya nguvu za kiroho ni mambo ambayo yapo hata sasa, na ni baadhi ya watu ndio wanaelewa habari hii vizuri na ni baadhi ya watu wachache wasio elewa habari hii ya nguvu za kiroho.


Watu hawa baadhi wanao elewa habari ya nguvu za kiroho na utendaji wake wanafahamu habari ya matambiko, na wanaelewa kuwa sio kila mahali pana stahili kufanyia matambiko, pia wanaelewa kabisa matambiko hujibu kwa muda na wakati sahihi.


Lakini pia watu hawa baadhi wasio elewa habari ya nguvu za kiroho sio makosa yao na wengine ni makusudi kabisa maana wanatumia vitu wasivyo vielewa wanaishi maisha wasiyo yaelewa pia na hawataki kuelewa kama hawaelewi.


Wanafahamu kuwa simu za mkononi na simu zingine hazifanyi kazi bila minara ya mawasiliano, lakini wengi wanaweza wasielewe kuwa sio kila mahari panafaa kuwekwa minara.


Watu wanao fahamu habari ya nguvu za kiroho wanaelewa kuwa sio kila mahali ni kitovu cha nguvu za kiroho sahihi kwa ajili ya matambiko na pia wanaelewa kuwa sio kila mahali panafaa kwa ajili ya minara ya mawasiliano.


Wakati huo huo hawa watu wasio elewa habari ya nguvu za kiroho wengi wao hawajui kuwa sio kila mahali pana stahili kuwekwa minara ya mawasiliano wao wapo wapo tu !.


Huu ndio utofauti wa jamii ya watu wanao elewa habari ya nguvu za kiroho, na wale wasio elewa habari ya nguvu za kiroho.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Watu wa kale walitumia wanyama mfano njiwa kufikisha ujumbe mahali pa mbali, na kwa mujibu wa o njiwa walifuata vitovu vya nguvu za kiroho kufika anapo elekea.


Vitovu hivyo vya nguvu za kiroho ndio hivyo au hapo sahihi kwa matambiko. 


Hata sasa watu wengi wasio elewa habari ya nguvu za kiroho hawaelewi kuwa sehemu nyingi walizo weka minara ya mawasiliano ni vitovu vya nguvu za kiroho.


Na pia hawana hata muda wa kujiuliza kuwa kati ya vitovu vya nguvu za kiroho na minara ya mawasiliano ni kipi kinaanza kuwepo.


Ni habari ya wazi kabisa kwamba dunia ina vitovu vya nishati za kiroho sehemu ambapo kwa watu wa kiroho wanaelewa utakatifu wa maeneo hayo, ambayo mara nyingi ni mlimani, kwenye miti ya aina flani, kwenye vya maji vya namna flani , na sehemu nyingine maalumu.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Sayari ya dunia ni kiumbe chenye uhai, ni hai kutokana maisha yanaendelea.


Kiumbe ni kitu chenye viungo, mfumo wa fahamu na kiumbe pia kina sehemu nyeti zake na hata sehemu ambazo kiumbe akiguswa anaweza kupoteza uhai wake.

Zaidi katika viumbe ni mfumo wa fahamu ambao kitaalamu wanaita mfumo wa neva.


Basi hata kiumbe sayari ya dunia ni hivyo hivyo kwa maana ya kuwa na vitovu vya nishati katika maeneo yake mbalimbali.


Elimu ya mashuleni wanaandika hilo pia na kufundisha habari ya mistari ya gridi katika somo la jiografia. Wakisema mistari ya gridi ni mistari ya kufikilika ya ulalo na wima na mistari hiyo hukutana katika maeneo maalumu na nilazima ikutane kutokana mingine ni wima na mingine ni ya ulalo.


Kwenye elimu ya shuleni wanafundisha ilipo kutana mistari hii ni sehemu maalumu lakini kwenye mafundisho ya kiroho sehemu hizo ndio vitovu vya nishati za kiroho.


Na makutano hayo ndio humo mara nyingi kuna shughuli za matambiko na minara ya mawasiliano.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Hata katika mtu sio kila mahali pana hatari au unyeti ndio hivyo hivyo kwa kiumbe sayari dunia.


Kidole cha mkono kina kazi lakini kikikatwa na kutolewa mtu hawezi kupoteza uhai wake, hata katika sayari ya dunia kuna vitovu vingi vya nishati za kiroho lakini vinazidiana umuhimu katika kuwepo.


Kwa mtu kichwa ni kiungo muhimu sana kwenye uwepo wa uhai wa mtu na mwili wake, hata kwa sayari ya dunia kuna sehemu ya muhimu au takatifu zaidi kama ilivyo kichwa kwa mtu.


Pamoja ni ukweli kwamba haiwezekani kukuta pweza wamezaliana na wanaishi mazingira ya mlimani pasipo na maji.

Hata katika maji sio kila mazingira utampata pweza.

Basi kila eneo huwa na vitu vyake kutokana na jinsi na namna lilivyo kwa asili yake.

Pia ni suala gumu kukuta jicho kwenye mguu bali ni rahisi zaidi jicho kuwepo kichwani kwa kiumbe.


Unaweza kuona kichwani ni patakatifu pa namna gani na ikiwa pweza kiumbe wa baharini na ni ngumu kupatikana sehemu pa nchi kavu pasipo na bahari na hata baharini sehemu za namna flani ndio pweza wapo, basi sehemu patakatifu pa sayari kiumbe dunia pata kuwa na vitu vya namna gani.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Tamaduni nyingi zenye hazina za thamani za kale zaidi zina elimu zake zenyewe. Lakini tamaduni za eneo flani katika sayari kiumbe dunia zinaonekana za kushangaza sana kuliko maeneo mengine.


Basi mtu unaweza kuelewa kwa urahisi mambo yote yaliyo endelea nayanayo endelea mashariki mwa bara la Afrika huko ambako kuna nchi ya Izraeli, huko kuliko nchi ya izraeli na maeneo yanayo zunguka eneo hilo.


Yapo mambo mengi ya mashariki huko.


Huko ni asili ya maandiko ya dini.

Huko kuna vita ambazo kimsingi haziishi tangu kale na hata sasa.


Huko ni kitovu cha nguvu za kir

oho, sehemu ambapo mkataba wa maisha ya kimwili na ukiroho ukifanyika kwa tambiko halali ni ngumu kuvunjwa na sheria tawala za mamlaka ndogo ndogo.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Post a Comment

0 Comments